Aunt Ezekiel & Wema Sepetu wawaomba msamaha Watanzania na Dunia kwa ujumla kwa kitendo chao cha kuvaa mavazi ya kudhalilisha
Wema Sepetu na Aunt Ezekiel walipokutana na waandishi wa habari leo
Aunt Ezekiel
Wema
Wema Sepetu na Aunt Ezekiel walipokuwa jukwaani katika tamasha la Fiesta mjini Dodoma
Mwigizaji wa filamu za kitanzania maarufu Bongo
Movie, Aunt Ezekiel amejitokeza mbele ya jamii na kuomba radhi juu ya kitendo
cha kuonyesha nguo za ndani katika tamasha la muziki lililofanyika mjini
Dodoma.
Akizungumza na waandihsi wa habari leo asubuhi mjini
Dar es Salaam, Aunt Ezekiel ambae alitakiwa kuandamana na msanii mwenzie
walioshiriki pamoja katika tamasha hilo la Fiesta Wema Sepetu ambae hakufika
kutokana na sababu ambazo hazikuwekwa wazi alisema anaiomba radhi jamii ya
watanzania kwani ilikuwa mara yao ya kwanza kushiriki tamasha lile na hakujua
urefu wa jukwaa na aina ya mavazi yatakayoweza kuwasitiri maungo yao tofauti na
wasanii wa kike wa muziki ambao walionekana kutambua matamasha hayo hivyo
kuweza kujisitiri vizuri.
“Unajua ile ni mara yetu ya kwanza wasanii wa Bongo
Movie kushirikishwa katika tamasha la Fiesta, hivyo hatukujua kama majukwaa
yanayotumiaka ni marefu sana kiasi mtu akiwa chini anaweza kuona nguo yako ya
ndani na kukufanya uonekane muhuni wakati sivyo ilivyo,” alisema Aunt Ezekiel
kwa huzuni.
Hata hivyo wakati akijibu maswali ya waandishi wa
Habari Ezekiel alionekana kubabaika baada ya Kidojembe kumuuliza kuwa anakunywa
pombe na kujikuta anakiri mbele ya
wanahabari kuwa alikuwa amekunywa pombe siku ya tukio hivyo kutotambua
alichokifanya. Lakini baada ya kuulizwa na Hemed Kivuyo kutoka Radio One, juu
ya hali ya ulevi Aunt Ezekiel alipinga kusema alikuwa amelewa.
“Naomba ieleweke, niliulizwa hapa kama nakunywa
nikajibu nakunywa, na nilipoulizwa tena kuwa siku ya tukio nilikunywa nikakiri
nilikunywa lakini hakuna mahali niliposema nimelewa. Nakiri siku hiyo
nilikunywa lakini sikuwa nimelewa,” alisisitiza Aunt.
“Ndugu waandishi wa habari pamoja na yaliyotokea
tunachukua fursa hii kuomba msamaha kwa wizara ya habari utamaduni na michezo,
shirikisho la filamu Tanzania, Bongo Movie Club na wadau wake, familia zetu na
jamii kwa ujumla kutokana na picha zilizopigwa tukiwa katka tamasha la Fiesta
mjini Dodoma ambazo zimesambazwa katika vyombo vya habari na mitandao ya
kijamii,” aliongeza Aunt Ezekiel kwa niaba ya msanii mwenzie Wema Sepetu.
Hata hivyo mwigizaji huyo maarufu kwa kuvaa viguo
vifupi aliweka wazi kuwa hatoacha kuvaa viguo vifupi ingawa hatofanya hivyo
katika hadhara bali atakuwa anaonyesha akiwa katika filamu tu.
“Mimi ni mwigizaji, zipo aina ya filamu zinakutaka
kuvaa nguo fupi siwezi kuacha lazima nifuate agizo la mwongozaji filamu hii ni
kazi yangu. Naomba msamaha katika jamii lakini naomba niweke wazi kuwa sitoacha
kuvaa nguo fupi,” Aunty.
Wakati akimalizia mkutano huo katibu wa shirikisho
la filamu Tanzania Wilson Mwakume, alisema kuwa Aunt Ezekiel amekwazwa sana na
tukio hilo hasa ikizingatiwa mwezi ujao anategemea kufunga ndoa na mchumba
wake, hivyo familia ya mchumba wake imejisikia vibaya baada ya kuona picha zile
katika vyombo vya habari. Na shirikisho lao lilipokaa katika kikao cha nidhamu
waliwaita wasanii hao na kuwataka waiombe radhi jamii na kuahidi kutorudia
kitendo hicho cha aibu.
No comments:
Post a Comment