UHUSIANO WA DAWA ZA KULEVYA NA VVU/ UKIMWI UKOJE?
Matumizi ya dawa za kulevya yanaongezeka kwa kasi nchini na hivyo huchangia kuleta madhara makubwa katika jamii yetu. Moja ya madhara hayo ni kuenea kwa vvu miongoni mwa watumiaji wa dawa hizo, wenzi wao na hata kusambaa kwenye jamii yote matumizi ya dawa za kulevya kwa wale waliokwisha ambukizwa vvu huongeza kasi ya kupatwa na ukosefu wa kinga (UKIMWI ) Mwilini hivyo kuambukizwa magonjwa nyemelezi kirahisi zaidi na kufa mapema .DAWA ZA KULEVYA ZINAWEZAJE KUENEZA VIRUSI VYA UKIMWI?
Matumizi ya dawa za kulevya huweza kueneza VVU kwa namna mbili tofauti:
.Kufanya ngono zisizo salama baada ya uwezo wa kufikiri na kutoa maamuzi wa mtumiaji kuathirika na dawa hizo.
.Kushirikiana sindano au mabomba au vifaa vingine vya kujidunga wakati wa kuzitumia dawa hizo.
Wakati vitendo hivi huwaweka watumiaji wa, dawa za kulevya katika hatari ya kupatwa na VVU na hata kuambukiza wengine .Tafiti zinaonesha kuwa ;
Mwaka 2004, 31.3% ya wanaojidunga kutoka katika jiji la dar es salaam waliambukizwa VVU.
TABIA HATARISHI NI ZIPI?
Mtu yeyote anayetumia dawa za kulevya hasa yule anayejidunga yupo katika hatari ya kuambukizwa VVUHata hivyo , Wale ambao huwa katika maeneo yenye utumiaji wa dawa za kulevya wana hatari zaidi ya kuambukizwa VVU kwa kufanya ngono zisizo/ salama na watumiaji dawa hizo .Aidha , vijana wenye umri
wa kupevuka wapo katika hatari zaidi ya kuambukizwa VVU kwa vile mara nyingi hujiingiza zaidi kwenye tabia nyingi ambazo humweka mtumiaji wa dawa za kulevya katika hatari kubwa ya kuambukizwa VVU zifuatazo ni baadhi tu ya tabia hizo ;
.Kutumia mara kwa mara na kwa muda mrefu dawa za kulevya
.Kushirikiana dawa au sindano au mabomba au vifaa vungine vya kujidunga ,
.Kusafisha vifaa vya kujidunga walivyoshirikiana bila kufuata taratibu zinazoweza kuua vijidudu
. kufanya ngono zisizo salama .
.Kuwa na wapenzi wengi (kubadilisha wapenzi ) kununua penzi kwa dawa au fedha,
.Kufanya mapenzi kinyume cha maumbile.
MAMBO GANI HUCHOCHEA TABIA HATARISHI?
Uelewa mdogo juu ya tabia zenyewe hatarishiMtazamo potofu kuwa kushirikiana sindano au mabomba ni ishara ya uaminifu na udugu miongoni mwa wanaojidunga
. misukumo rika
. arosto kali inayotokana na utegemezi
.Kuzoeleka kwa matumizi ya dawa za kulevya katika jamii zetu
.Ugumu wa maisha
HATUA GANI ZICHUKULIWE KUZUIA MAAMBUKIZI YA VVU?
Kiongozi
. Kuweka sera zisizikandamize ,zisizobagua na zisizowatenga watu wanaotumia dawa za kulevya ili wawezekuzifikia huduma za tiba.
.kuelimisha umma juu ya tatizo la dawa za kulevya na maambukizi ya VVU .
.kuhakikisha programu za kuwasaidia watumiaji wa dawa za kulevya zinaanzishwa na kuendelezwa .
Mwananchi:
Kutowanyanyapaa na kutowabagua watumiaji wa dawa za kulevya na badala yake kuwachukulia kuwa watumiaji ni watu wanaohitaji msaada wa matibabu na kuwaelekeza sehemu watakapozipata huduma za tibaMtumiaji wa dawa za kulevya :
Kuacha kutumia dawa za kulevya.Kuacha kushirikiana sindano au mabomba au vifaa vingine vinavyotumika kujidunga .
.Kusafisha vyema vifaa vya kujidunga kwa kuchemsha au kutumia dawa za kusafishia
No comments:
Post a Comment