SIMU ZAZIMWA NCHI NZIMA KENYA
Tume ya mawasiliano kenya kuzima simu feki za kichina mikononi mwa watu, hazifanyi kazi tena
Stori kubwa Kenya ambayo hata kwenye AMPLIFAYA ya CLOUDS FM october 1
2012 imeshika nafasi ya kwanza ni kuhusu mamlaka ya mawasiliano nchini
Kenya kuzizima kiteknolojia simu zote zilizofeki ambazo zimekua
zikitumiwa na wakenya.
Mtangazaji wa Citizen Tv/Radio William Tuva ameripoti kwamba wakenya
walionunua simu feki wapo kwenye wakati mgumu na itawabidi wanunue simu
original kwa sasa ili kurudi tena kwenye mawasiliano.
Ameripoti pia kwamba inasemekana katika mtandao wa simu za mkononi wa
Safaricom peke yake ni wateja laki sita ambao wameripotiwa simu zao
kuzimwa kwa sababu ni feki.
Kwenye line nyingine Tuva ameripoti pia kwamba Kenya imepoteza mabilioni
ya shilingi kutokana na simu feki ambazo zimekua zikiingia sokoni kwa
njia ambayo sio halali.
Baadhi ya wananchi ambao simu zao zimefungwa wamekaririwa wakisema
waliamka asubuhi na kukuta simu zao hazifanyi kazi, kumbe tayari
zimeshazimwa kiteknolojia na tume ya mawasiliano nchini humo ambapo kwa
mujibu wa BBC n wateja milioni mbili na nusu ambao simu zao zimezimwa.
Mmoja wa watu hao amekaririwa akisema “usiku ninawekaga alamu nataka saa
11 niamke, sikusikia naamka tu naona nje kunapambazuka na simu yangu
wamezima’
No comments:
Post a Comment