Wednesday, October 3, 2012

MBUNGE WA KAWE,HALIMA MDEE, ATAKA NYUMBA YA MCHUNGAJI LAKWATARE IBOMOLEWE


Serikali imetakiwa kumdhibiti na kumuondoa, kisha kuibomoa nyumba ya Mbunge wa Viti Maalum (CCM), Mchungaji Getrude Lwakatare.
Rai hiyo imetolewa na Waziri Kivuli, Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi ambaye pia ni Mbunge wa Kawe (Chadema), Halima Mdee.
Taarifa kwa vyombo vya habari jana ilieleza kuwa, wakati raia wengine wakibomolewa nyumba ambazo kama ilivyo ya Mchungaji Lwakatare, zilijengwa kinyume cha sheria, Mbunge huyo amehamia na kuishi kwenye nyumba yake.
Julai mwaka huu, nyumba za wananchi waliojenga katika maeneo tengefu ya ufukwe wa Jangwani, mto Ndumbwi na mto Mbezi, zilibomolewa katika operesheni iliyoendeshwa na Baraza la Mazingira la Taifa (Nemc).
Operesheni ambayo ilihusisha takriban nyumba 15 na kuta nane. Lakini nyumba ya Mchungaji Lwakatare haikuguswa


No comments:

Post a Comment