NINI MAANA YA UKATILI WA KIJINSIA
Ni kitendo cha ukatili kuhusu jinsia ambacho kinaweza kusababisha madhara / maumivu ama mateso ya kimwili au kisaikolojia kwa mtu ikiwa ni pamoja na vitendo vya kutishia ,kulazimisha kunyima uhuru,bila kujali vimefanyika kisiri ama kwenye kadamnasi".
NB: ukatili wa kijinsia huhusishwa na ukatili kwa wanawake kwani wao ndio waathirika zaidi wa ukatili.
AINA ZA UKATILI WA KIJINSIA
kuna aina nyingi za ukatili wa kijinsia .
UKATILI WA KUTUMIKA NGUVU
kupigwa makofi ,mateke ,
kuchapwa
kutupia au kupigwa na vitu vya ndani
UKATILIWA KISAIKOLOJIA
kusema mambo yanayomfanya mtu kujisikia mdogo,
kunyanyasa
kusimangwa
kudhalilisha
kuwekwa chini yake,kukuweka mbali na ndugu au marafiki .
UKATILI WA KIUCHUMI
kunyimwa mahitaji muhimu na fedha za kujikimu ,
kunyimwa umiliki wa mali,
kuzuiwa kufanya kazi.
UKATILI WA KIUTAMADUNI NA MILA KANDAMIZI
Ndoa za utotoni .
utakasaji na kurithi wajane ,
Mauaji ya vikongwe.
Ukeketaji
UKATILIWA KINGONO
kubakwa
kulawitiusafirishwaji wa watu wanawake na watoto
kukushika bila ya ridhaa
HALI YA UKATILI WA KIJINSIA TANZANIA
kutokana na taarifa ya demographic health survey 2010 inaonesha tatizo limekuwa , linakuwa na linakithiri katika sehemu zote za tanzania
UKATILIWA KUTUMIA NGUVU
zipo taarifa zinaonesha 61% ya wanawake walioko kanda ya kati hufanyiwa aina hii ya ukatili ,na 22% ya wanawake wa kanda ya kaskazini.
UKATILI WA KINGONO
taarifa zinaonesha kuwa ,mkoa wa mara unaongoza kwa 48.1% na mikoa mingine ni kama ifuatavyo : kigoma (31.9%),mbeya (30.8%), ruvuma (30.4%) na rukwa (30.2%).
UKATILI WA KIUCHUM
32.56% ya wanawake wanakumbwa na ukatili huu ,kwa kunyimwa haki ya kumiliki ardhi na mali nyingine.
NANI HUFANYA UKATILI WA KIJINSIA?
ukatili wa kijinsia hufanywa na Baba , mama ,mke ,shemeji , baba mkwe, mama mkwe, shangazi, mjomba ,dada ,kaka, nk.
MAPENDEKEZO ILI KUONDOA UKATILI WA KIJINSIA
Tanzania imeridhia mikataba ya kimataifa inayopinga ukatili wa kijinsia .mikataba hii ni kama mkataba wa A frika wa haki za binadamu na haki za watu ,Mkataba wa Nyongeza wa haki za wanawake (2003) ,Mkataba
wa kuondoa .Aina zote za ubaguzi dhidi ya wanawake -CEDAW(1979),na mengineyo.hivyo basi ,ili kuweza kutekeleza mikataba hii na kuwalinda wanawake dhidi ya ukatili ,tanzania inatakiwa
- .kutunga sheria ambayo itakataza itakataza ukatili wa kijinsia wa aina zote ikiwemo ukatili wa kutumia nguvu ,ngono,saikolojia nk kuunda vituo vya kuhifadhi waathirika wa ukatili .,
- .Kuunda vituo vya ushauri nasaa wa kifamilia juu ya ukatili na kusaidia waatirika kurudi katika hali yao ya kawaida .
- Kujenga mazingira ya kupewa msaada wa haraka kwa wahanga kwa kuanzisha ngazi za serikali za mitaa; vijiji mpaka serikali kuu,
- Kuweka mifumo ya kuwapatia msaada wa sheria kwa wahanga wa ukatili n.k
- Kutengeneza mazingira ya kuwaelimisha wanajamii wa marika yote madhara na athari za ukatili wa kijinsia hasa kwa wanawake na watoto wa kike
- Kuanzisha jitihada za kutoa elimu katika ngazi zote na kuelezea umuhimu wa kuhelimisha haki za Binadamu na haki za wanawake kwa misingi ya kuondoa ukatili.
No comments:
Post a Comment