Thursday, September 27, 2012

SOIL EROSION(MMONYOKO WA UDONGO)

                       MMOMONYOKO WA UDONGO(SOIL EROSION) 


Mmonyoko wa udongo ni kitendo cha  tabaka la juu la ardhi kuondole kutoka sehemu moja na kupelekwa mahali pengine na mawakala wa umomonyoaji(agents of erosion) baada ya tabaka la juu la ardhi kuachwa bila kufunikwa.
agents of erosion huchukua nafasi yao ya kumomonyoa udongo pale inapotokea ardhi hiyo imehujumiwa(degraded) kwa aidha shuguli za binadamu au kimazingira kwa kutokutambua au makusudi.uchunguzi unaonyesha kuwa asilimia kubwa ya mmonyoko wa udongo unasababishwa na shughuli za binadamu katika harakati zake za kujinasua kimaisha aidha kiuchumi,kijamii au kilimo.
Viwakala vya mmomonyoko wa ardhi hivi ni a) maji-water b)upepo-wind c)na barafu-ice.Maji,barafu,upepo unaokimbia baada ya ardhi kuachwa wazi husomba udongo wa mahali husika na kusababisha madhara ya kiikolojia ya mahali husika na madhara mengine hufuata ikiwemo ardhi kukoa rutuba,staervation,jangwa ,mabadiliko ya tabia ya nchi,kufa kwa viumbe hai(death of biodiversity) nk.

Zifuatazo ni sababu muhimu zisababishazo soil erosion

1. DEFFORESTATION(ukataji miti ovyo),hii ni moja ya sababu zisababishazo mmonyoko wa udongo kwa kukata miti ambayo hufanya tabaka la ardhi kufunikwa na kuushikamanisha udongo ardhini.Inaonyesha miti mingi hukatwa na wananchi wa kawaida katika shughuli kama za uandaaji mashamba,kujipatia nishati kama kuni,mkaa nk

2.SETTING BUSH FIRE(uchomaji moto misitu)  misitu huchomwa moto katika shughuli za binadamu kama uwindaji na kile ambacho kinaonyesha kuwa mila na desturi zilizopitwa na wakati ya kujipima umri kwa baadhi ya watu vijijini kuchoma moto ikiwaashiria kuwa jinsi utavyowaka ndo jinsi atavyoishi

3.BAD FARMING METHODS(mifumo mibaya ya ulimaji) mifumo mibaya ya ulimaji kama vile kilimo cha kuhamahama(shifting cultivation,pastoralism) huhamasisha ukataji wa miti ovyo kwani mkulima kila mwaka huhama eneo moja-shamba na kuliandaa kwa kukata miti na mwaka unaofuata vilevile hivyo huacha sehemu kubwa ya udongo haijafunika hivyo huwa rahisi kumomonyolewa na agents of erosion na kuicha ardhi hiyo haina thamani tena

4.OVERGRAZING(ufugaji wanyama wengi kupita kiasi) ufugaji wa wanyama wengi kupita kiasi katiaka eneo husika hulifanya eneo hilo kuwa halina misitu na hata ardhi yake kuwa loose hvyo basi kumeng'enywa kirahisi.

5.CONSTRUCTION OF INFRASTRUCTURES(ujenzi wa miundo mbinu) kipindi cha ujenzi wa miundo mbinu kama nyumba,viwanda,reli na barabara huchangia ukataji wa miti ovyo.

6.MINING ACTIVITIES(shughuli za uchimbaji madini) shughuli za uchimbaji madini husababisha uchimbaji wa ardhi na ukataji miti pia hivyo basi ardhi inakuwa unprotected


                  ZIFUATAZO NI ATHARI ZA MMONYOKO WA ARDHI
zifuatazo ni athari kuu za soil erosion 

1.JANGWA(DROUGHT)
kutokana na kukata miti ambako kutakuwa endelevu huacha ardhi haijafunikwa na kumomonyolewa na mwishowe kusababisha kubadilika kwa tabia nchi ya mahali husika ambapo kwakuwa miti huchangia upatikanaji wa mvua eneo husika 

2.KUBADILIKA KWA TABIA YA NCHI(climatic change)
miti na misitu kiujumla ni kitu muhimu sana katika kuchangia mvua na halijoto ya mahali husika(geoecolology) kwa sababu hufyonza kiasi kikubwa cha hewa ya carbon na kutoa oksijeni kwa viumbe hivyo basi mimea na wanyama hutegemeana na kufanya balansi ya ekolojia ya mahali husika.kitendo cha ukataji miti ovyo husababisha mmomonyoko wa ardhi na baadae kusababisha imbalance ya mazingira na viumbe vyake.

3.DEATH OR MIGRATION OF BIODIVERSITY (VIFO AU UHAMAJI WA VIUMBE)
kutokana na sababu za kiikolojia zisababishwazo pale soil erosion inapotokea husbabisha viumbe hai wa mahali husika kufa au kuhama

4.LOSS OF SOIL FERTILITY(ardhi kupoteza rutuba)
kutokana na kumomonyolewa kwa tabaka la juu la udongo, udongo hupoteza virutubisho muhimu ambavyo hufanya miti au mazao kutoweza kustawi. Hi ni kwa sababu tabaka la juu la udongo ndio ambalo huwa na virutubisho vingi katika udongo.
5.NJAA(STARVATION)
kutokana na athari zisababishwazo na soil erosion kama mabadiliko ya tabia nchi,ukame na ardhi kupoteza rutuba husababisha uzalishaji mdogo wa mazao na pengine njaa katika mahali husika na kuigharimu nchi au taasisi husika kununua chakula . 


PICHA ZIKIONYESHA MMOMONYOKO WA UDONGO NA ATHARI ZAKE
File:Regenerosion offenerBoden Tagebau.jpg

 










4 comments: