UTEUZI WA RAIS KIKWETE
Teuzi Za Rais Kikwete Tangu Alipoingia Madarakani
Wakuu naomba tuzitazame teuzi
za Kikwete tangu alipoingi madarakani. Teuzi hizi ziwe za viongozi wote
wa idara, wizara, sekta na taasisi muhimu serikalini walioteuliwa na
Rais - kasoro mawaziri, wakuu wa mikoa na wilaya.
Rais Jakaya Mrisho Kikwete, amemteua Jaji Mohamed Chande Othman kuwa Jaji Mkuu wa Tanzania,kuanzia tarehe 28 DIsemba, 2010.
Rais Jakaya Mrisho Kikwete, amemteua Bwana Deos Khamisi Mndeme kuwa Posta Masta Mkuu wa Shirika la Posta Tanzania. 26/09/2012
Rais Jakaya Mrisho Kikwete, amemteua Ndugu Said Mwema kuwa Inspecta Generali wa Polisi Tanzania,kuanzia tarehe 3 march, 2006.
Rais wa Jakaya Kikwete amemteua
Bi. Hawa Magongo Mmanga kuwa Mwenyekiti mpya wa Bodi ya Wakala wa
Barabara nchini (TANROADS) kwa kipindi cha miaka mitatu. 25/09/2012
Rais Jakaya
Mrisho Kikwete, amemteua bwana Othman Rashidi kuwa Mkuu wa Kitengo cha
Usalama wa Taifa Tanzania,kuanzia mwezi August, 2006.
Rais Jakaya MrishoKikwete amemteua Bwana Rished Bade kuwa Naibu Kamishna Mkuu wa Mamlakaya Mapato Tanzania (TRA). 19/09/2012
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete amemteua BIBI MWANAHAMISI OMARI KITOGO kuwa MSAIDIZI WA RAIS, HUDUMA ZA JAMII. 08/05/2012
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa
Tanzania, Mheshimiwa Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete amemteua Bwana Ignus
Paul Kitusi kuwa Msajili Mkuu wa Mahakama (Chief Registrar) kuanzia
tarehe 1 Julai, 2012.
Rais Jakaya Mrisho Kikwete
amemteua Bwana Hussein A. Kattanga kuwa Mtendaji Mkuu wa Idara ya
Mahakama kuanzia tarehe 1 Julai, 2012.
RAIS Jakaya Kikwete amemteua Salim
H. Msoma kuwa Mwenyekiti wa bodi ya kampuni ya Ndege Tanzania ATCL.
Uteuzi huo umeanza maramoja Juni 22, 2012.
Rais Jakaya Kikwete, amemteua Winfrida Beatrice Korosso, kuwa Katibu wa Tume ya Kurekebisha Sheria nchini. 14/08/2012
Aidha, Mhe. Rais amemteua Bwana
Benedict Bartholomew Mwingwa kuwa Msajili wa Mahakama Kuu (Registrar of
the High Court) kuanzia tarehe 1 Julai, 2012.
RAIS Jakaya Mrisho Kikwete ameteua wakurugenzi wapya tisa wa Wizara ya
Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa ambao pia watakuwa na hadhi ya
balozi. Uteuzi huo umeanza Mei 2, mwaka huu.Walioteuliwa ni Vincent
Kibwana ambaye anakuwa Mkurugenzi, Idara ya Afrika; Naimi Aziz
(Mkurugenzi, Idara ya Ushirikiano wa Kikanda); Celestine Mushy
(Mkurugenzi, Idara ya Ushirikiano wa Kimataifa); Yahya Simba
(Mkurugenzi, Idara ya Mashariki ya Kati), na Bertha Somi ambaye
ameteuliwa kuwa Mkurugenzi, Idara ya Diaspora.Wengine ni Irene Kasyanju
(Mkurugenzi, Kitengo cha Sheria); Dorah Msechu (Mkurugenzi, Idara ya
Ulaya na Amerika); Mbelwa Kairuki (Mkurugenzi, Idara ya Asia na
Australia) na Silima Haji ambaye ameteuliwa kuwa Mkurugenzi, Idara ya
Mambo ya Nje, Zanzibar.
No comments:
Post a Comment