Maprofessor WATATU WAKUBALIANA TANZANIA HAMNA DEMOCRASIA
MADA ILIKUWA NI TANZANIA BAADA YA MIAKA 20 YA VYAMA VINGI(MULTIPARTISM)
Mada hiyo ilikuwa ikijadiliwa katika kipindi maalum cha TBC THIS WEEK IN PERSPECTIVE ambacho kilirushwa hewani jana tar 28.september 2012 majaira ya saa tatu usiku kiliwaalika wadau ambao tunaweza kusema wana ushawishi mkubwa kisiasa kwa kuwa ndio watu waasisi wa elimu ya siasa tanzania na hata wengine wameshawahi kuitumikia serikali katika nyakati fulani.
Waalikwa hao walikuwa ni prof. max muya, political scientist university of dar es salaam , dr Hassy kitine, prof. Gaudance Mpangala, na Judge Justice Thomas Mihayo ambaye ni retired judge of high court.
katika mazungumzo hayo mmoja wapo wa waheshimiwa hao Prof. Muya alionyesha kulitalawa jukwaa hilo kwa kutoa historia ya democratic waves ya Samuel Herrington na kufafanua kuwa dunia imepitia awamu tatu za mabadiliko ya kidemokrasia kuanzia miaka ya 1800 katika nchi za america na ulaya ya magharibi na awamu ya pili ni ile ya nchi za asia kama india nk na sisi Africa tumefanya mabadiliko ya kidemokrasia tukiwa watu wa mwisho miaka ya 1980s mbali na maelezo hayo alifafanua nguzo(pillars) kuu za demokrasia za Demokrasia sambamba na kuzungumzia kuwa Demokrasia ni ustaarabu wa watu wa jamii ya kikristo na unahusisha mabadiliko ya hatua za kiuchumi na kijamii.
Katika nguzo hizo za demockrasia zilipochanganuliwa ndipo Maprof; hao wengine walipochangia na kuendeleza kuchambua huku wakitoa reference katika nchi yetu a Tanzania
Pillars hizo za demokrasia ni pamoja na
Accountability(Uwajibikaji) hasa wa maafisa wa juu kabisa wa serikali ikiwemo mawaziri.manaibu n.k suala ambalo ukiingalia katika nchi yetu ni kitendawili katika kulitekeleza hili willingly na nchi za kiafrica kiujumla.
Intergrity(uaminifu)tumeshuhudia viongozi wengi tu wakituhumiwa rushwa ,uharamia nk katika hili huikosesha Afrika na Tanzania kiujumla kuwa nchi zinazoendeshwa kideokrasia.
Purity and discretion(uhusikaji katika shughuli ambazo ni za kiserikali moja kwa moja na sio za kisiasa) katika nguzo hii Dr. Hassy Kitine alitolea mifano ya watu kufa katika mazingira ambayo yanahisisha politics na Prof. Gaudence Mpangala ndipo alipodakia na kutoa element za serikali ambazo hazifuati nguzo hizi ni pamoja na kujihusisha kwa maafisa wa kijeshi,taasisi mbalimbali,wakuu wa mikoa wilaya n.k katika siasa moja kwa moja kukipendelea chama kinachotawala .Alisema watu pia lazima wapewe uhuru wa kueleza mawazo yao kitu ambacho nchi kama Tanzania wapo watu ambao wanamamlaka ya kuizuia haki hiyo yote haya ni kwa sababu serikali ilyopo madarakani inahofia mabdiliko!,lakini kuhusiana na suala hili kidogo Judge Justice Thomas Mihayo alionyesha kidogo kutofautiana na wenzake akitolea mfano kuwa siku hizi hata mtu ambaye ni masikini anawez kutoa mawazo yake ikilinganishwa na miaka ya 80,ingawa kuna baadhi ya sehemu kama bungeni haki hii imeonekana kuzuiliwa
Na freedom to compete(uhuru wa kushindana)ilifafanuliwa kuwa serikali ya kidemokrasia ni ya kishindani na lazima kuwe na uhuru wa kushinda pia Dr. Hassy Kitine aliongeza kuwa kitu hiki serikali ngingi za kiafrika hazipendi kusikia wanajitahidi kila njia kuwazuia wapinzani .
No comments:
Post a Comment