Wakuu naomba tuzitazame teuzi za Kikwete tangu alipoingi madarakani. Teuzi hizi ziwe za viongozi wote wa idara, wizara, sekta na taasisi muhimu serikalini walioteuliwa na Rais - kasoro mawaziri, wakuu wa mikoa na wilaya.


Rais Jakaya Mrisho Kikwete, amemteua Jaji Mohamed Chande Othman kuwa Jaji Mkuu wa Tanzania,kuanzia tarehe 28 DIsemba, 2010.

Rais Jakaya Mrisho Kikwete, amemteua Bwana Deos Khamisi Mndeme kuwa Posta Masta Mkuu wa Shirika la Posta Tanzania. 26/09/2012


Rais Jakaya Mrisho Kikwete, amemteua Ndugu Said Mwema kuwa Inspecta Generali wa Polisi Tanzania,kuanzia tarehe 3 march, 2006.



Rais wa Jakaya Kikwete amemteua Bi. Hawa Magongo Mmanga kuwa Mwenyekiti mpya wa Bodi ya Wakala wa Barabara nchini (TANROADS) kwa kipindi cha miaka mitatu. 25/09/2012

Rais Jakaya Mrisho Kikwete, amemteua bwana Othman Rashidi kuwa Mkuu wa Kitengo cha Usalama wa Taifa Tanzania,kuanzia mwezi August, 2006.

Rais Jakaya MrishoKikwete amemteua Bwana Rished Bade kuwa Naibu Kamishna Mkuu wa Mamlakaya Mapato Tanzania (TRA). 19/09/2012


Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete amemteua BIBI MWANAHAMISI OMARI KITOGO kuwa MSAIDIZI WA RAIS, HUDUMA ZA JAMII. 08/05/2012

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete amemteua Bwana Ignus Paul Kitusi kuwa Msajili Mkuu wa Mahakama (Chief Registrar) kuanzia tarehe 1 Julai, 2012.


Rais Jakaya Mrisho Kikwete amemteua Bwana Hussein A. Kattanga kuwa Mtendaji Mkuu wa Idara ya Mahakama kuanzia tarehe 1 Julai, 2012.


RAIS Jakaya Kikwete amemteua Salim H. Msoma kuwa Mwenyekiti wa bodi ya kampuni ya Ndege Tanzania ATCL. Uteuzi huo umeanza maramoja Juni 22, 2012.


Rais Jakaya Kikwete, amemteua Winfrida Beatrice Korosso, kuwa Katibu wa Tume ya Kurekebisha Sheria nchini. 14/08/2012


Aidha, Mhe. Rais amemteua Bwana Benedict Bartholomew Mwingwa kuwa Msajili wa Mahakama Kuu (Registrar of the High Court) kuanzia tarehe 1 Julai, 2012.


RAIS Jakaya Mrisho Kikwete ameteua wakurugenzi wapya tisa wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa ambao pia watakuwa na hadhi ya balozi. Uteuzi huo umeanza Mei 2, mwaka huu.Walioteuliwa ni Vincent Kibwana ambaye anakuwa Mkurugenzi, Idara ya Afrika; Naimi Aziz (Mkurugenzi, Idara ya Ushirikiano wa Kikanda); Celestine Mushy (Mkurugenzi, Idara ya Ushirikiano wa Kimataifa); Yahya Simba (Mkurugenzi, Idara ya Mashariki ya Kati), na Bertha Somi ambaye ameteuliwa kuwa Mkurugenzi, Idara ya Diaspora.Wengine ni Irene Kasyanju (Mkurugenzi, Kitengo cha Sheria); Dorah Msechu (Mkurugenzi, Idara ya Ulaya na Amerika); Mbelwa Kairuki (Mkurugenzi, Idara ya Asia na Australia) na Silima Haji ambaye ameteuliwa kuwa Mkurugenzi, Idara ya Mambo ya Nje, Zanzibar.