Tuesday, December 25, 2012

JWTZ WAMSAKA ASKARI ALIYEPIGA PICHA NA GODBLESS LEMA KATIKA MJI MDOGO WA MARERANI-MANYARA





JWTZ WAMSAKA ASKARI ALIYEPIGA PICHA NA GODBLESS LEMA KATIKA MJI MDOGO WA MARERANI-MANYARA.

Kwa ufupi
‘‘Kimsingi Jeshi linafanya uchunguzi wa kumtambua mtu huyo kama kweli ni askari,’’ ilisema sehemu ya taarifa ya Kurugenzi ya Habari na Uhusiano ya jeshi hilo ambayo iliyatilia shaka mavazi aliyokuwa amevaa mtu huyo kama ndiyo yanayotumiwa na jeshi hilo sasa.
 Mtu aliyejitambulisha kuwa askari wa Jeshi la wananchi wa Tanzania (JWTZ),kambi ya Monduli,Arusha akiwa na wabunge wa Chadema,Godbless Lema (Arusha Mjini) na Joshua Nassari (Arumeru Mashariki) baada ya kumalizika kwa mkutano wa hadhara uliohutubiwa na wabunge hao katika Mji mdogo Mererani,Simanjiro mkoani Manyara.  

WAKATI Jeshi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ), likihaha kumtafuta aliyepiga picha na Mbunge wa Arusha Mjini (Chadema), Godbless Lema akiwa amevaa sare za jeshi hilo, mtu huyo ameibuka na kusema yuko tayari kufukuzwa kazi kuliko kuacha kuishabikia Chadema.

Kauli hiyo ya JWTZ imekuja baada ya jana, gazeti hili kuchapisha picha ya mtu huyo aliyejitambulisha kuwa ni askari wa JWTZ akiwa amepiga picha na Lema pamoja na Mbunge wa Arumeru Mashariki, Joshua Nassari, huku akiwa amenyoosha vidole viwili alama inayotumiwa na Chadema.

Baada ya taarifa hiyo, JWTZ lilitoa taarifa likieleza kushtushwa na tukio hilo na kusema kwamba linamtafuta mtu huyo kwa udi na uvumba ili kujiridhisha kama kweli ni askari wake.

‘‘Kimsingi Jeshi linafanya uchunguzi wa kumtambua mtu huyo kama kweli ni askari,’’ ilisema sehemu ya taarifa ya Kurugenzi ya Habari na Uhusiano ya jeshi hilo ambayo iliyatilia shaka mavazi aliyokuwa amevaa mtu huyo kama ndiyo yanayotumiwa na jeshi hilo sasa.

Taarifa hiyo ya JWTZ, ilisema ingekuwa rahisi kumtambua mtu huyo kwa kuangalia paji la uso lakini alilifunika ili asitambulike.

‘‘Pamoja na hayo, jeshi linamtafuta ili kumchukulia hatua za kinidhamu kutokana Kanuni za Majeshi ya Ulinzi likisema Sheria namba Nne ya Mabadiliko ya Nane katika Katiba ya Nchi ya mwaka 1992, Ibara ya 147(3), mwanajeshi yeyote hatakiwi kujihusisha na masuala ya kisiasa,’’ ilisema taarifa hiyo.

Mbali ya taarifa hiyo, Msemaji wa JWTZ, Kanali Kapambala Mgawe alisema endapo itabainika kuwa aliyevaa sare hizo ni mwanajeshi, moja ya hatua dhidi yake ni kufukuzwa kazi mara moja.

Mbali na hatua hiyo, Kanali Mgawe alisema kuanzia sasa, Jeshi limepiga marufuku mtu yeyote kuvaa sare zake katika mikutano yote ya siasa na atakayebainika atachukuliwa hatua kali za kinidhamu.

Kuhusu kitendo cha askari huyo kupiga picha na Lema, Kanali Mgawe alisema moja ya masharti muhimu ya askari anapiojiunga na jeshi ni kutambua na kutii sheria inayomzuia kujihusisha na masuala ya siasa na kwamba kitendo cha mtu huyo kimemshangaza na kumfanya amtilie shaka kama kweli ni askari aliyekamilika.

Msimamo wa mtuhumiwa:

Kwa upande wake, mtu huyo aliyejitambulisha kuwa ni askari wa Kikosi cha Chuo cha Mafunzo Monduli (TMA), mkoani Arusha, alisema ni bora afukuzwe kazi kuliko kunyimwa kujiunga na Chadema.

Akizungumza jana kwa sharti la kutotajwa jina akiwa Mirerani, Simanjiro mtu huyo alisema Chadema ni chama makini chenye uwezo wa kuongoza nchi kwani kinatetea wanyonge na kujali masilahi ya jamii.

Friday, December 21, 2012

U SHONE LIKE DIAMONDS 2012




BREAKING NEWZZZZ!!!!!!! LULU WA KANUMBA AACHIWA,X MASS NA MWAKA MPYA UNAKULA URAIANI



BREAKING NEWZZZZ!!!!!!! LULU WA KANUMBA AACHIWA,X MASS NA MWAKA MPYA UNAKULA URAIANI

Msanii wa filamu nchini elizabeth Michael(lulu) ambaye aalikamatwa kwa kosa la mauaji ya Msanii mwenzake Steven kanumba na kesi yake kuchukua muda mrefu sana hadi juzi ilipo ripotiwa kuwa amesomewa mashitaka ya kuua bila kukusudia,

Tetesi hai kutoka mahakamani zinadai kwamba ameachiwa kwa dhamana kwa sababu anahukumiwa kesi ya maaujai bila kukusudia.
Hukumu inayodaliw akutolewa asubuhi hii Tar 21/12/2012 ni kwamba hakimu ameruhusu Lulu kuachiwa kwa dhamana.
Kama ni kweli kwamba Lulu ameachiwa huru ni dhahili X mass na mwaka mpya Lulu atakula akiwa uraiani
TAARIFA KAMILI ZA UKWELI WA HABARI HII KUKUJIA HIVI PUNDE

Mbunge wa Arusha mjini Godbless lema ameshinda rufaa yake ya ubunge.



Habari zilizotufikia hapa mtandaoni kutoka kwa mtu wetu aliyepo mahakamani ni kwamba Mbunge wa Arusha mjini Godbless lema ameshinda rufaa yake ya ubunge.
Rufaa hiyo ilikuwa inasikilizwa mahakama kuu ya rufaa jijini Dar es salaam.Kwa maaana hiyo ni kwamba lema kwa sasa atakuwa mbunge halali wa arusha mjini.

Ikumbukwe lema alisimamishwa ubunge wake kupitia kesi iliyofunguliwa kwamba wakati wa kampeni zake alitoa lugha isisiyotakiwa kwa mgombea wa ccm.