Zitto kabwe atinga polisi,aandikisha statement kufuatia kutishiwa maisha
Zitto kabwe atinga polisi,aandikisha statement kufuatia kutishiwa maisha
Nimetoka makao makuu ya polisi, upelelezi, kuandika statement
kuhusu vitisho dhidi yangu kufuatia hekaya inayoitwa "Ripoti ya Siri ya
Zitto Kabwe". Chanzo cha hekaya sasa kinabadilishwa kutoka makao makuu
ya CHADEMA na kuwa ni usalama wa Taifa au CCM. Wahusika waendelee
kuhamisha chanzo lakini wajue watasakwa na kukamatwa na kuburuzwa
mahakamani. Nimewashitaki kwa kunitishia maisha. Ninawashitaki kwa
kunichafua kwa tuhuma za uongo.
Ninafanya haya kwa lengo la kuhakikisha kuwa siasa za kuzushiana na kusambaza uongo zinakuwa na gharama kubwa.
source; Zitto Kabwe facebook account
My take movie inaendelea bila shaka Yericko Nyerere,Ben Saanane na Theo
Mutahaba mjiandae kuja kukamatwa kwa jinsi ninavyowafahamu polisi wa
Tanzania wameshapata sababu ya kuwasotesheni Jela
No comments:
Post a Comment