Tuesday, November 12, 2013

Hizi ni allegations za mh zitto kwa theo mutahaba baada ya kushtukia mchezo mzima wa ripoti ya siri


Tumeshajua huyo anayejiita Theo mutahaba ni mganga njaa mmoja aliye karibu na watu wenye nyadhifa. Jina hilo feki lakini hana akili kwani katumia kompyuta yake na kirahisi teknolojia imemnasa. Mwisho wa uongo ni aibu. Mahakama na uchunguzi makini utaokoa watanzania dhidi ya wanasiasa waongo. Vifaranga na mama zao watawajibishwa kisheria na jamii

TUJIULIZE NA KUTAFAKARI: Ikiwa, Kwa mujibu wa Sheria ya Usalama wa Taifa Na. 15/1996 ni wajibu wa TISS kukusanya, kuchunguza, kuchambua na kuhifadhi taarifa za kiuchunguzi/kijasusi ambazo ni hatarishi kwa usalama wa taifa, na kwamba baada ya kupata taarifa hizo wataishauri serikali au taasisi husika ya serikali(s. 15); IKIWA, Kwa Mujibu wa kifungu cha 16 cha sheria hiyo ni marufuku kwa mtu yeyote ambaye pasi na idhini ya kimaandishi kutoka kwa Waziri mwenye dhamana ya Usalama wa Taifa(UWT) kimaandishi, kuchapisha au kuruhusu kuchapisha katika gazeti au penginepo pale, ukweli kwamba fulani ni mfanyakazi wa Usalama wa taifa (zaidi ya Mkurugenzi Mkuu) au anahusika na Usalama wa taifa; IKIWA, kwa mujbu wa kifungu cha 17 cha sheria hiyo, taarifa za kijasusi zinazopatikana wakati wa upepelezi ni siri na mtu yeyote anayezipata wakati akifanya kazi hiyo ya kiupelelezi haruhusiwi kuzitoa hadharani isipokuwa tu kwa mujibu wa sheria na/au idhini ya Waziri, na taarifa hizo sana sana hutolewa kwa viongozi wa serikali wenye dhamana ya upepelezi au AG na ikiwa kukaidi kufanya hivyo ni kukiuka kiapo cha utii kwa mfanyakazi yeyote yule wa TISS; Na Ikiwa kujifanya wewe ni afisa usalama wa taifa au unafanya kazi kwa maelekezo ya usalama wa taifa ni kosa kisheria, JE?
(a) Watu kama Theo Mutahaba wanapata wapi Mamlaka ya (i) kujinadi kwamba wao wanafanya kazi na UWT (ii) Wao wamehusika katk ujasusi uliohusisha TISS na ktk kumlambisha mzigo Zitto Kabwe
(b) Ikiwa itabainika kuwa watu kama Theo Mutahaba sio wafanyakazi wa idara hiyo muhimu kwa usalama wa nchi, je watu kama hao wanajua madhara haya kisheria?
(c) Serikali ya nchi masikini kama Tanzania inaweza kutumia zaidi ya Bil. 250 kumhonga mtu kama ZZK ili anyamaze kwa maslahi yapi ya taifa? je? ZZK ana nguvu gani kuwafanya watumie hela zote hizo waache kutengeneza madawati, wakati he is just an ant to arrest?
(d) Ni Kweli watu kama Dr. Kitila Mkumbo wa pale mlimani wanaweza kuwa cheap kuhongwa laki mbili mbili? (if thats true tumekwisha)
(e) Je, kiwango cha juu cha kuchukua pesa Western union ni kiasi gani kwa siku?
(d) Ikiwa ni kosa kutaja majina ya waajiriwa wa UWT na hata wale wanaohusiana nao zaidi ya Mkurugenzi mkuu je? hawa watu wanaowataja mbona wanaachwa? is this by accident or by design?
Msando Alberto, John Seka, Juma Kibacha,Kitila Mkumbo, Euseby John, Robert Lengeju,

SOURCE;zzk facebook profile https://www.facebook.com/zittokabwe?hc_location=stream

No comments:

Post a Comment