Tuesday, May 27, 2014

Mbunge wa Nkasi mh. Ally Kessy asema Wazanzibar wanachosha, ni mzigo

Mbunge wa Nkasi Mheshimiwa Kesi amesema imetosha sasa kubeba mzigo wa Wazanzibar ambao kwa miaka 20 hawachangii chochote zaidi ya Tanzania bara kuchangia kila kitu harafu wao hawatoi chochote!

Anasema wanataka tugawane mambo yote sawa kwa gharama za kodi ya watu wa bara,anasema wabunge wazanzibar wanapata mfuko sawa wa jimbo wakati majimbo yao madogo ukipiga flimbi wananchi wote wanasikia jimbo zima!

Anasema Watanzania tumechoka kuwatunza wazanzibar waende zao na umeme hawalipi deni lakini wao ndio vinara wa kulalamika!

No comments:

Post a Comment